Skip to main content
Humanities LibreTexts

8.1: Muhtasari na Mchezo: Sura ya nane

 • Page ID
  79941
 • An audio element has been excluded from this version of the text. You can listen to it online here: http://pb.libretexts.org/kiswahili/?p=210

  Morogoro T.T.C. ilikuwa shule yenye majengo mazuri sana wakati Rosa alipoingia. Wanafunzi walikuwa wachache. Wasichana walikuwa wachache zaidi. Rosa alipofika hakuwa na nia tena ya kutafutamchumba. Sasa alipenda kupendeza kila mvulana. Alijulikana kwa kila mvulana. Rosa alipopata mimba, alijaribu kuitoa. Alilazwa hospitali. Alipotoka aliendelea na ‘mchezo’ wake tena. Wavulana walimwita “Lab”.

  An audio element has been excluded from this version of the text. You can listen to it online here: http://pb.libretexts.org/kiswahili/?p=210

  Mama yake alipopata habari  kwamba Rosa alijifungua mtoto wa kiume, alimwandikia Rosa kwa furaha. Kumbe, haikuwa kweli. Rosa alipata barua nyingine kutoka Flora. Flora naye alikuwa amekwisha toa mimba.

  An audio element has been excluded from this version of the text. You can listen to it online here: http://pb.libretexts.org/kiswahili/?p=210

  Rosa sasa alikuwa amejulikanaMorogoro nzima. Mwishowe sifa yake iliwafikiamapadri wa pale. Padri mmoja alitumwa aende kumwonyesha mwanga wa wokovu. Alipokuja aliona kitabu cha Rosa kilichoeleza habari za mapenzi, vidonge vya kuzuia mimba, furaha ya mwili, na kadhalika. Padri akaanza kuhubiri akisema, “Nimekuletea habari njema, Rosa.” Alianza kumsomea Rosa sehemu ya Bibliainayozungumziamwanamke asherati. Alimwambia, “Rosa, wokovu uko bado machoni mwako!” Lo! Rosa alikasirika sana. Alisema kwamba maisha yake yalikuwa yamekwisha haribika, akamfukuzaPadri.

  Rosa hakujali kabisa.  Aliendelea tu na maisha yake ya umalaya.

  Exercises

  The original version of this chapter contained H5P content. You may want to remove or replace this element.

   

  • Was this article helpful?